Yupo mungu wa upendo
Pamoja twamuita Baba
Mwenye familia na upendo
Asiye na mwanzo wala mwisho
Mungu mwenye haki
Muumba wa mbingu
Huwapa haki watu wote
Tumaini la mwisho kwa watu
Watu wa dunia hii
Tangu mi nikujue sio Yule
Umerudisha mengi kwangu, ndio
Bwana ninakusifu
Naimba halleluya
Utukuzwa milele yote
Nimerudishiwa na bwana
Thamani ya uzima yangu
Siwezi hesabu
Siwezi kuhesabu
Matendo na wema ya mungu
Nimerudishiwa na Yesu
Zaidi ya jana na juzi
Sasa ninakiri
Ninashuhudia kuna mungu
Mungu wa watu
Utumwa wa yusufu
Bwana uliondoa
Kamvika na heshima, kapanda kapanda
Kawa mheshimiwa
Bwana uliondoa shida za yusufu tukuzwe
Nilipolemewa na mizigo
Moyo ukajawa na simanzi, hee
Ukanirudishia furaha yangu
Ukanijaza Baraka na uzima
Nimerudishiwa na bwana
Thamani ya uzima yangu
Siwezi hesabu
Siwezi kuhesabu
Matendo na wema ya mungu
Nimerudishiwa na Yesu
Zaidi ya jana na juzi
Sasa ninakiri
Ninashuhudia kuna mungu
Mungu wa watu
Najua najua kwamba wewe
Ni mungu uliye mwaminifu
Kwamba, mambo yote warudisha
Nilivyopoteza
Bado mi huomba huomba
Sijawahi kuchoka
Nakuamini pekee, pekee Yesu
Wanipenda ndio maana
Warudisha vingi vilivyo vyangu
Nimerudishiwa na bwana
Thamani ya uzima yangu
Siwezi hesabu
Siwezi kuhesabu
Matendo na wema ya mungu
Nimerudishiwa na Yesu
Zaidi ya jana na juzi
Sasa ninakiri
Ninashuhudia kuna mungu
Mungu wa watu
Leave a Reply